Binti wa Will Smith na Jada Pinkett, Willow Smithamesema mafanikio yake ambayo ameyapata, hayahusiani kwa namna yoyote na familia yake
Binti wa Will Smith na Jada Pinkett, Willow Smith ameweka nyongo kali kwenye mioyo ya wafuatiliaji na wapenzi wa familia yao, amesema mafanikio yake ambayo ameyapata, hayahusiani kwa namna yoyote na familia yake.
Willow ambaye ana umri wa miaka 24, amesema wazazi wake hawahusiki kwenye mafanikio ambayo ameyapata. Kitoto hicho cha 2000 hadi sasa kimefanikiwa kuachia Album 7, na kucheza filamu zaidi ya 10.
Jina lake limetajwa kwenye Tuzo mbali mbali ikiwemo Grammy Awards, MTV, na kushinda Tuzo kadhaa ikiwemo BET Award






