P-Diddy kubaki katika jela za gereza la ‘Metropolitan Detention Center’ lililopo Brooklyn nchini Marekani
Jaji Arun Subramanian amelitupilia mbali ombi la dhamana toka kwa Sean “Diddy” Combs na timu yake ya wanasheria. Ameshauriana na waendesha mashtaka kuwa aendelee kubaki katika jela za gereza la ‘Metropolitan Detention Center’ lililopo Brooklyn nchini Marekani wakati akisubiri hukumu yake ambayo ni Oktoba 3 mwaka huu.
Diddy aliiomba mahakama dhamana kwa kuweka rehani fedha kiasi cha ($50 million) na kuahidi kubaki nyumbani ndani ya jumba lake mjini Miami, pia kutosafiri nje ya Florida na New York lakini Jaji amelitupilia mbali ombi hilo.
Rapa huyo wa Marekani alikamatwa tarehe 17 Septemba 2024 na kushtakiwa kwa utumwa wa kingono na utapeli na waendesha mashtaka wa New York.






