Zari the Boss Lady alipoteza Ujauzito wake 2026
Mume wa socialite maarufu Zari The Boss Lady, Shakib Chams, kwa uchungu ameweka wazi tukio la kusikitisha ambapo mke wake alipoteza ujauzito wao mwezi Mei mwaka huu. Kwa mujibu wa Shakib, Zari alikuwa na ujauzito wa takribani wiki sita kabla ya mimba hiyo kuharibika.
Shakib amesema tukio hilo lilikuwa na athari kubwa kihisia kwao kama wanandoa, na kwa neema za Mwenyezi Mungu, kama mambo yangeenda salama, Zari angejifungua mtoto wao mapema mwaka 2026.








