Naymar Aachiwa Urithi wa Trilioni 2.5 na Mtu Asiye Mjua.

Naymar Aachiwa Urithi wa Trilioni 2.5 na Mtu Asiye Mjua.

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Brazil Naymar Jr amepata zari la Mentali baada ya mwanaume mmoja asiyemfahamu wala kuwahi kukutana nae kuandika jina lake kama mrithi wa mali zake

Mwanaume huyo Bilionea mwenye umri wa miaka 31 ambaye mpaka sasa jina lake halijafahamika ameandika urithi huo wa Naymae kurithi utajiri wake wa zaidi ya Dola za Marekani Bilioni 1 ambazo ni sawa na zaidi ya Shilingi Trilioni 2.5 za Kitanzania huku akidai kuwa anampenda sana Naymar jinsi ambayo si mbinafsi na jinsi ambavyo anamjali sana baba yake mzazi.

Bilionea huyo anasema upendo wa Naymar kwa baba yake mzazi unamkumbusha jinsi ambavyo yeye aliishi na baba yake enzi za uhai wake. Jamaa huyo anatajwa kutokuwa na mtoto wala mke.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button