Azua Taharuki Kwa Kujenga Kijiji cha Wake zake 39 na Watoto wake 94

Azua Taharuki Kwa Kujenga Kijiji cha Wake zake 39 na Watoto wake 94.

Kwenye milima ya Mizoram, India, aliishi mwanaume ambaye maisha yake yaligeuka hadithi ya Dunia nzima. Nyumba yake haikuwa tu makazi-ilifanana na kijiji kidogo kutokana na ukubwa wa familia yake isiyo ya kawaida.

Umaarufu wake ulianza mwaka 2011 baada ya kuripotiwa kuwa anaishi chini ya paa moja na wake zake 34, jambo lililowashangaza wengi. Kadri miaka ilivyoenda, familia hiyo ilikua hadi kufikia watoto 94 na wajukuu 33, wote wakiishi pamoja ndani ya jengo la ghorofa nne lililoangalia mji wa Baktawng.

Familia hii ilifuata mafundisho ya dhehebu la kienyeji lililoanzishwa na baba yake, na yeye mwenyewe aliheshimiwa kama kiongozi wa kundi hilo. Alipofariki dunia mwaka 2021, si wakazi wa Mizoram pekee bali watu kutoka India nzima na mataifa mengine walitafakari juu ya maisha yake ya kipekee maisha yaliyounda jamii kubwa kutokana na imani ya familia pana na kuishi kwa pamoja.

Tukio hili linabaki kuwa mfano wa ajabu wa namna mtu mmoja anavyoweza kuacha alama ya kipekee, akiiacha jamii ya Watu wengi, aliyoianzisha mwenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button