Mgodi Waporomoka na Kuuwa Watu 32.
Mgodi Waporomoka na Kuuwa Watu 32.
Daraja katika mgodi wa cobalt ulioko Lualaba, kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limeporomoka na kusababisha vifo vya wachimbaji 32 wa kujitegemea
.Afisa wa serikali ya mkoa amesema ajali hiyo ilitokea Jumamosi katika sehemu ya mgodi iliyokuwa imefurika. Waziri wa mambo ya ndani wa mkoa huo, Roy Kaumba Mayonde, amesema juhudi za uokoaji zinaendelea kutafuta manusura au miili zaidi. Zaidi ya watu 200,000 hufanya kazi katika migodi mikubwa ya cobalt isiyo rasmi nchini humo.





