Tunataka Kujua ni Haki Gani Vijana wanadai
Tunataka Kujua ni Haki Gani Vijana wanadai.
“Kwa ufupi nataka kusema yafuatayo kwanza nadhani Tume tunatarajia ikatuangalizie sababu hasa iliyoleta kadhia ile ni nini? Kiini cha tatizo ni nini? Na wakati inatokea kadhia ile vijana waliingizwa barabarani kudai Haki? Tunataka kujua haki gani?Ambayo vijana hawa wameikosa na kwa umoja wao waliingia barabarani kuidai haki hiyo lengo la wale vijana kuingia barabarani ili tuweze kuifanyia kazi na wapate haki yao.” Amesema
“Tunapokwenda kufanya hii kazi twende tukaangalie matamshi ya vyama vya upinzani wale waliokuwa wakisema lazima kiwake, hapakaliki, lazima aondoke, lazima kiwe hiki uchaguzi hautafanyika kitu gani hadi kilichowaletea kufanya vile lakini katika kufanya hivo tuangalie uhusiano wa hicho chama Tume yetu ya Uchaguzi, uhusiano wao ulikuwaje katika kipindi hicho mpaka ikawapelekea waseme maneno yale.” Amesema Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Tume ya Uchunguzi wa yaliyotokea Octoba 29.





