Apata Ugonjwa Hatari Kisa Kuzidisha Kunywa Energy Drink’s
Apata Ugonjwa Hatari Kisa Kuzidisha Kunywa Energy Drink's
Kisa cha Artem, kijana mwenye umri wa miaka 22 kutoka St. Petersburg, Urusi, kimezua mjadala mkubwa kuhusu madhara ya matumizi kupita kiasi ya energy drinks. Awali alianza kwa kopo moja kwa siku, lakini muda ulivyoenda, utegemezi ukaongezeka hadi makopo 3-5 kwa siku, mara nyingi akiwa hajala chochote na akicheza michezo ya kompyuta kwa muda mrefu.
Baada ya muda mfupi alianza kulalamika maumivu makali ya tumbo, kutapika na kichefuchefu. Madaktari waligundua ana pankreatitis, ugonjwa unaoathiri kongosho. Licha ya matibabu, tatizo liliendelea kurudi mara kwa mara hadi uvimbe ukaanza kukua kwenye kongosho.
Wakati wa kulazwa kwa mara ya tatu, hali yake ilizidi kuwa mbaya, Artem alikumbwa na purulent necrosis, aina hatari ya kuharibika kwa tishu za kongosho, ikifuatiwa na sumu kusambaa mwilini. Madhara hayo makubwa yalisababisha kupooza miguu, na hivyo kupoteza uwezo wa kutembea.
Kwa sasa, kijana huyo yuko kwenye hatua ya rehabilitation, akijifunza upya jinsi ya kusimama na kutembea, huku madaktari na familia wakitumaini ataweza kurejea katika hali yake ya kawaida.
Kisa cha Artem kinakuwa onyo kali kwa vijana na watu wanaotegemea energy drinks kupita kiasi, hasa wanaokunywa wakiwa na njaa au kutumia kama njia ya kuongeza nguvu wakati wa kazi nyingi, au kusoma usiku kucha. Kunywa bila mipaka kunaweza kuleta madhara ya muda mrefu, na kwa baadhi, kunaweza kubadilisha maisha kabisa.





