Huwezi Kumpatia Mtu Msamaha Kama Hajakiri Kosa.

Huwezi Kumpatia Mtu Msamaha Kama Hajakiri Kosa.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametuma ombi kutaka kupatiwa msamaha wa rais kwa kesi ya rushwa inayomkabili ambapo hatua hiyo imezua ukosoaji mkali kutoka kwa wapinzani na makundi ya kupigania ya demokrasia nchini humo ambayo yamemrai Rais Isaac Herzog kutolikubali ombi hilo.

Kiongozi wa upinzani, Yair Lapid ni miongoni mwa wale wanaopinga Netanyahu kupatiwa msamaha, siku moja baada ya waziri mkuu huyo kuwasilisha ombi rasmi la kusamehewa kwa kesi inayomwandama.

Wapinzani wake wamesema iwapo litakubaliwa litautia doa mfumo wa utoaji haki na taasisi za kidemokrasia na kuonesha kana kwamba Netanyahu yuko juu ya utawala wa sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button