Miaka 35 Sio Umri Wamwisho Kuoana na Kufanikiwa Kimaisha
Miaka 35 Sio Umri Wamwisho Kuoana na Kufanikiwa Kimaisha
Michelle Obama na Barack Obama wamekuwa mfano wa upendo, umoja na uongozi kwa zaidi ya miaka 33 tangu walipofunga ndoa tarehe 3 Oktoba 1992. Safari yao kutoka Chicago hadi Ikulu ya White House imejenga urithi mkubwa unaoendelea kuhamasisha mamilioni ya watu duniani, hasa vijana na watu wazima wanaopambana kujitengenezea maisha bora.
Lakini leo, Michelle Obama amerejea tena kwenye vichwa vya habari kwa ujumbe ambao unaodai “Miaka 35 sio mwisho wa kutimiza kila kitu ikiwemo ndoa na mafanikio mengine ya kimaisha-usijistress!
Kupitia podcast yake “The Look”, akiwa na Jane Fonda na Bethann Hardison, Michelle alifunguka kuhusu ushauri angeutoa kwa toleo lake la miaka 35. Alisema huu ni umri ambao wengi huanza kujilinganisha na wenzao, kuamini kuwa kazi zao zingepaswa kuwa mbali zaidi, au kuhisi muda unawapita kwenye masuala kama ndoa, familia na mafanikio ya kibinafsi.
Lakini Michelle anasema: “furahia umri huo, jifunze kupitia changamoto zake, na acha kujilazimisha kufikia milestones ambazo jamii imeweka.
Ni ujumbe unaoendana kabisa na safari yao ya maisha na ndoa, kwamba kila mtu ana ratiba yake, na ukuaji wa kweli haupimwi kwa umri, bali kwa uwezo na ubunifu.
Kwa kifupi, ikiwa unafikiria kuwa 35 ni mwisho, Michelle Obama anakuambia “Hapana. Umri huo ni mwanzo wa kukua, kuelewa na kujitengeneza.”





