Mbappé afikia rekodi ya Mabao 59 ya Cristiano Ronaldo akiwa Real Madrid.

Mbappé afikia rekodi ya Mabao 59 ya Cristiano Ronaldo akiwa Real Madrid.

Mbappé ameandika historia mpya ndani ya Santiago Bernabéu kwa kufikia rekodi ya Cristiano Ronaldo ya kufunga mabao 59 katika mwaka mmoja wa kalenda akiwa Real Madrid, rekodi iliyowekwa na CR7 mwaka 2013. Mbappé alifanikisha hilo kwa mtindo wa kipekee, na akisherehekea mafanikio hayo kwa kushangilia kwa style ya “SIUUU” ishara ya heshima kwa mchezaji aliyekuwa ndoto yake tangu utotoni.

Kisa cha Mbappé kinagusa mioyo ya wengi. Kwani akiwa mtoto, chumba chake kilijaa picha za Cristiano Ronaldo akiwa amevaa jezi ya Real Madrid. Leo, ndoto hiyo imegeuka kuwa uhalisia si tu kuvaa jezi hiyo maarufu, bali pia kusawazisha rekodi ya idol wake ndani ya klabu hiyo hiyo.

Rekodi ya magoli mengi zaidi kwa Real Madrid ndani ya mwaka mmoja wa kalenda sasa inasomeka hivi: Cristiano Ronaldo (2013): mabao 59

NEW

Kylian Mbappé (2025): mabao 59

Cristiano Ronaldo (2012): mabao 58

Mbappé ameonyesha wazi kuwa ukuu hutambua ukuu, na kwamba kizazi kipya kinaweza kuheshimu kilichotangulia huku kikitengeneza historia yake yenyewe. Real Madrid imeshuhudia wakati adimu ambapo jana na leo vinakutana na soka linashinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button