Halima Ahmad Kopwe Kuiwakilisha Tanzania Miss World.
Aliyekuwa Miss Tanzania mwaka jana 2022 @halimakopwe anatarajiwa kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya Dunia “71st Miss World’ yatakayofanyika Delhi nchini India December 09, 2023.
Taarifa iliyotolewa @misstanzaniaorganisation imesema Warembo wote akiwemo Halima watapokelewa November 08,2023 kwa ajili ya kuanza kambi rasmi ya mashindano hayo kwa muda wa mwezi mmoja kabla ya Fainali.
Siku chache kabla ya kuanza safari Miss Tanzania anatarajiwa kukabidhiwa bendera ya Tanzania na Waziri mwenye dhamana kwenye hafla ya kuagwa rasmi mwisho wa mwezi October.
Mbali na kwenda kushindana Halima atatumia fursa hii kutangaza utalii na Taifa la Tanzania katika jukwaa la Dunia.