Kumekucha,Trump Kuwatimua Wahamiaji Marekani.
Kumekucha, Trump Kuwatimua Wahamiaji Marekani.
Katika mahojiano yake ya kwanza tangu
apate ushindi wake, Rais Mteule wa Marekani Donald Trump alisema hakuna mjadala juu ya mipango yake ya kufukuza wahamiaji nchini humo.
Miongoni mwa vipaumbele vya Trump, cha kwanza ni kuimarisha ulinzi wa mpakani, hivyo amesema utawala wake hauna “budi” ila kuwarejesha makwao wahamiaji hao akidai kuwa hilo ndio litakuwa suluhisho.
Suala la uhamiaji ni miongoni mwa sera
iliyomfanya apate ushindi huo, na Trump alisema kuwa na wapiga kura wa Marekani, walikuwa wanatafuta mgombea atakayewasaidia Wamarekani kwa maarifa.