Muhimbili Yakanusha Wagonjwa 25 Kufa Kila Siku Mloganzila.
Muhimbili Yakanusha Wagonjwa 25 Kufa Kila Siku Mloganzila.

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imetolea ufafanuzi wa taarifa iliyochapishwa kupitia Mtandao wa JamiiForums umechapisha taarifa yenye kichwa cha habari “Serikali imulike Hospitali ya Mloganzila, huduma zake ni janga kwa wagonjwa na ndugu wanaouguza.’
Kutokana na taarifa hiyo, Uongozi wa Hospitali imetolea ufafanuzi.
Taarifa hiyo ambayo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Aminiel Buberwa Aligaesha imefafanua habari hiyo iliyochapishwa na mtandao wa Jamii Forums kuwa wagonjwa 20 hadi 25 kufariki kwa siku Miaka ya hivi karibuni hadi Novemba 21, 2024,
Idadi ya wagonjwa wanaoonwa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeongozeka kutoka wagonjwa wa nje 400 hadi 1,000 kwa siku na idadi ya wagonjwa waliolazwa wodini wakati wote imeongezeka kutoka 200 hadi 400 kwa siku.
Hii ni kutokana na uboreshaji mkubwa wa mifumo na huduma uliofanywa hospitalini hapo na hatimaye kuvutia wananchi wengi kuitumia hospitali hiyo.
Idadi ya wagonjwa wanaofariki kwa siku hospitalini hapo kutokana na sababu mbalimbali ni kati ya wanne (4) hadi sita (6) kati ya wagonjwa 400 waliolazwa na siyo 20 hadi 25 kwa siku kama ilivyoelezwa katika taarifa iliyochapishwa na JamiiForums.






