Mbowe na Wenzie 10 Waachiwa kwa Dhamana

Mbowe na Wenzie 10 Waachiwa kwa Dhamana

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe pamoja na wanachama wengine kumi, akiwemo Mwenyekiti Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Songwe Bw.Elia Zambi, wameachiwa kwa dhamana huku Jeshi la Polisi likiendelea kumshikilia kada wa chama hicho Bw. Mdude Nyagali.

Akizungumza mara baada ya kushikiliwa kwa saa kadhaa na kuachiwa majira ya usiku Mbowe anasema Jeshi la Polisi mkoani Songwe limesema linamshikilia Mdude kutokana na kuwa na mashitaka mengine dhidi yake, huku wao wakitakiwa kurudi kituoni hapo novemba 29 mwaka huu.

Ikumbukwe kuwa Mbowe na wenzake kumi na moja walikamatwa novemba 22, 2024 katika eneo la Halungu wilayani Mbozi mkoani Songwe, kwa madai ya kuharibu ratiba ya mikutano ya kampeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button