Ndumbaro ziarani katika Kampuni ya kuzuia uhalifu na uvamizi kwa njia ya mtandao kwenye viwanja vya michezo ya “Positive Technology”
KUELEKEA AFCON 2027 MHE. NDUMBARO APIGA HODI KAMPUNI YA “CYBER” URUS
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro @damasndumbaro_official amefanya ziara katika Kampuni ya kuzuia uhalifu na uvamizi kwa njia ya mtandao kwenye viwanja vya michezo ya “Positive Technology” iliyopo Jijini Moscow nchini Urusi kwa lengo la kuona na kujifunza namna teknolojia hiyo ivyotumika.
Mhe. Ndumbaro amefanya ziara hiyo Desemba 1, 2024 ikiwa ni sehemu mikakati ya maandalizi ya fainali za michuano ya Mashindano ya AFCON mwaka 2027, ambayo itafanyika kwa kushirikiana na Kenya na Uganda ambapo mifumo hiyo itasaidia kuimarisha ulinzi, kulinda mifumo ya huduma kama vile umeme, maji, matangazo, kuingia na kutoka pamoja dharura viwanjani na katika mikusanyiko mbalimbali ya watu.
Katika ziara hiyo Mhe. Ndumbaro ameambatana na Makamu wa kwanza wa rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) Athumani Nyamlani ambaye amesema kuwa mifumo hiyo itasaidia kuongeza usalama katika maeneo viwanja na kukuza ubora wa ligi kuu ya Tanzania.
Urusi ina uzoefu wa mifumo hiyo katika maeneo ya viwanja kufuatia uenyeji wao wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 ambazo zilifanyika kwa mafaniki