Meek Mill Aibuka Kumtetea Diddy “HAKUFANYA HAYO YOTE”
Meek Mill Aibuka Kumtetea Diddy "HAKUFANYA HAYO YOTE"
Rapa MeekMill aibuka na kumkingia kifua rafiki yake Rapa #Diddy ambae kwa sasa anakabiliwa na mashtaka mengi ya unyanyasaji wa Kijinsia na Biashara ya ngono.
Kupitia ukurasa wake wa X amefunguka kuwa yote yanatokea kwa sababu wao ni watu weusi na anamtakia kheri Diddy alipo na anaamini hakufanya yote ambayo anaambiwa kafanya.
Pia alishare baadhi ya Blogs ambazo zimekuwa zikipost mara kwa mara taarifa Za #Diddy na kusema kuwa zinafanya hivyo kwa sababu hazimilikiwi na watu weusi hivyo wanafanya ili kuua majina ya watu weusi.
Mbali na hivyo Meek ameahidi kudeal na yeyote ambae itagundulika yupo nyuma ya kinachoendelea.