Siri Yakuishi Muda Mrefu ni Kunywa Bia Bila Ndoa

Siri Yakuishi Muda Mrefu ni Kunywa Bia Bila Ndoa.

Katika umri wa miaka 105, Kathleen Hennings anasema siri ya maisha yake marefu ni kufurahia bia na kutowahi kuolewa.

Akiwa mzaliwa wa Brixton mwaka 1919, alisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwenye nyumba ya wazee huko Cheltenham, akiwa ameshika glasi ya bia yake pendwa.

Kathleen aliishi maisha yake akifanya kazi kama mhasibu mjini London, akitumia jioni zake kucheza kwenye Covent Garden na kuhudhuria opera na ballet kabla ya kuhamia Cotswolds mwaka 1965.

Mtazamo wake kuhusu maisha marefu ni wa kipekee na unapingana na tafiti zinazodai ndoa huongeza umri wa kuishi, akionesha kwamba furaha na utimilifu wa maisha hupatikana kwa njia nyingi tofauti.

Unauonaje ushauri wake?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button