Wanawake Ambao Hawapo Kwenye Mahusiano Wanafuraha Kuliko Wanaume.
Wanawake Ambao Hawapo Kwenye Mahusiano Wanafuraha Kuliko Wanaume.
Utafiti uliochapishwa katika jarida la Social Psychologicaland PerSonality Science umegundua kuwa wanawake wasio na wapenzi wanapata ustawi wa juu wa maisha ukilinganisha na wenzao wa kiume.
Wanasaikolojia wa Chuo Kikuu cha Toronto, Elaine Hoan na Geoff MacDonald, walichambua takwimu kutoka kwa takriban watu 6,000 waliokuwa single, wengi wao wakiwa ni wa jinsia tofauti.
Utafiti ulionesha kuwa wanawake waliripoti kuridhika zaidi na maisha na mahusiano ya ngono, huku wakionesha hamu ndogo ya kuwa na mwenza.