Anaedai Kubakwa na Jay-z Atoa Maelezo Tofauti.
Anaedai Kubakwa na Jay-Z Atoa Maelezo Tofauti

Jane Doe, anayewashutumu Jay-Z na Diddy kwa ubakaji alipokuwa na miaka 13, amekiri uwepo makosa kwenye kumbukumbu zake. Alisema sio sura zote zilikuwa wazi na anaweza kuwa alikosea kuwatambua wahusika.
Baba yake amekanusha madai kwamba alimsafirisha baada ya tukio, akisema hakumbuki safari hiyo ya masaa matano.
Wakili wa Jane Doe, Tony Buzbee, alisema baba huyo alikuwa na changamoto zake binafsi wakati huo.
Jane Doe pia alidai kuzungumza na Benji Madden kwenye after-party ya VMAs 2000, lakini NBC ilithibitisha kuwa Benji hakuwepo kwenye tukio hilo.
Jay-Z ameita madai hayo ya uwongo na ya kutafutia umaarufu, huku wakili wake akiomba kesi hiyo ifutwe.
Jane Doe, akiungwa mkono na wakili wake, amekubali kufanyiwa kipimo cha polygraph kuthibitisha madai yake.





