Waziri Bashungwa awasili makao makuu ya polisi na ziara ya kikazi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa leo tarehe 22 Januari 2025 amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP. Camillus Wambura pamoja na Makamishna wa Jeshi hilo

Katika ziara hiyo ya kwanza ya Kikazi katika Jeshi la Polisi tangu alipoteuliwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri Bashungwa amepokelewa kwa salamu ya gwaride la heshima (Mounted Guard).

Pamoja na Mambo mengine, Waziri Bashungwa atafanya kikao na kuzungumza na Maafisa, Wakaguzi, Askari wa  vyeo mbalimbali na Watumishi wengine wa Jeshi la Polisi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button