Lissu Afika Kwenye Uchaguzi Mkuu Chadema na Gari Alilopigwa Nalo Risasi.

Lissu Afika Kwenye Uchaguzi Mkuu Chadema na Gari Alilopigwa Nalo Risasi.

Mgombea Uenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, amekuwa wa kwanza kuwasili katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaa, ambapo leo Januari 21, 2025 unafanyika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa juu
wa chama hicho.

Lissu amewasili katika viwanja vya ukumbi huo saa 10:15 asubuhi, akiwa ndani ya gari jeusi Land Cruiser lenye namba za usajili T216 DHH.

Baada ya kufika, alipokelewa kwa shangwe na wafuasi wake waliokuwa wameshika mabango huku wakiimba, “Lissu! Lissu!”
Wafuasi hao pia wamesukuma gari lake hadi eneo la maegesho kabla ya mgombea huyo kuingia ukumbini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button