20 Wakamatwa Kwakula Mchana wa Ramadhani

20 Wakamatwa Kwakula Mchana wa Ramadhani

Polisi wa Kiislamu katika jimbo la Kano, kaskazini mwa Nigeria wamewakamata Waislamu 20 waliokutwa wakila mchana hadharani wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambapo pia Watu watano wamekamatwa kwa kuuza chakula huku Naibu kamanda Polisi Mujahid Aminudeen akisisitiza kuwa msako huo utaendelea mwezi mzima.

Aminudeen amesema hatua hiyo inalenga kudumisha heshima ya Ramadhan kwani Waislamu wanapaswa kufunga kuanzia alfajiri hadi jua linapozama pia ameeleza kuwa wale waliokamatwa tayari wamefikishwa katika Mahakama ya Sharia kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mbali na hilo Polisi wa kiisalmu wa Hisbah pia wamewakamata Watu waliovaa mavazi yanayokiuka maadili ya Kiislamu wakiwemo waliokuwa na nywele zisizoruhusiwa na Madereva wa Bajaji waliowachanganya Abiria wa jinsia tofauti.

Mfumo wa Sharia umeendelea kutumika katika baadhi ya majimbo ya kaskazini mwa Nigeria kwa Waislamu tangu kuanzishwa kwake zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button