Yanga – Mrithi wa Joseph Guede huyu Hapa
Klabu ya @yangasc Inaelekea kukamilisha Usajili wa Mshambuliaji raia wa Ghana Jonathan Sowah (24),
Makubaliano binafsi baina ya Mchezaji Jonathan Sowah na klab ya Yanga yalikwisha kamilika na kinachoelekea Mwisho kwasasa ni Makubaliano baina ya klab yake ya Al-Nassr Benghazi ya Libya na Uongozi wa klab ya Young Africans,
Kwa mujibu wa Chanzo chetu kutoka Ghana kimethibitisha kuwa Usajili huu unatarajiwa kukamilika Wikiend hii na Jumalijalo Sowah atatua Nchini Tanzania kuungana na waajiri wake wapya hao Young Africans,
Sowah alijiunga na klab ya Al-Nassr Benghazi ya Libya kwa Mkataba wa Miaka Miwili (2) akitokea Nchini Ghana katika klab ya Medeama ambapo Mpaka sasa ameshatumikia Miezi 6 tu,
Klab ya Yanga Inaelekea kumpa Mkataba wa Mkopo wa Msimu Mmoja huku endapo wataridhishwa nae basi watakuwa na room ya kuketi na kumuongezea zaidi muda wa kuendelea kusalia klabuni hapo.







