Trump amshukia Papa Leo XIV kuhusu Iran

Trump amshukia Papa Leo XIV kuhusu Iran

mwananchi_official Rais wa Marekani, Donald Trump amemshambulia vikali kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Pope Leo XIV, akimtuhumu kuunga mkono Iran kuwa na silaha za nyuklia.

Kauli hiyo ya Trump imekuja baada ya Papa Leo XIV, ambaye ni papa wa kwanza kutoka Marekani, kuendelea kukosoa vita vinavyoendelea kati ya Marekani, Israel na Iran, pamoja na kupinga kuenea kwa silaha za nyuklia duniani.

Kupitia ujumbe wake katika mitandao ya kijamii, Trump alimuita papa huyo kuwa dhaifu katika sera za usalama na mambo ya nje, akisisitiza kuwa hataki kiongozi wa dini anayeonekana kuruhusu Iran kumiliki silaha za nyuklia.

Hata hivyo, msimamo wa Papa Leo XIV umekuwa wazi, akipinga vikali vita na matumizi ya nguvu, huku akisisitiza kuwa Mungu haungi mkono migogoro na suluhu ya kudumu ni mazungumzo ya amani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button