Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amekutana na mwenzake wa Ukraine Dmytro Kuleba
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amekutana na mwenzake wa Ukraine Dmytro Kuleba wakati wa ziara ya Kyiv, ya kushtukiza mapema Jumatano. Blinken aliwasili Kyiv kufuatia usiku wa mashambulizi ya anga ya Russia yaliyosababisha vifo vya takriban watu 16. Hii ni ziara yake ya nne tangu Moscow ilipoanza uvamizi wake dhidi ya Ukraine. Afisa mmoja wa wizara ya mambo ya nje amewaambia waandishi habari walipokuwa wanaelekea Kyiv kwamba, Marekani itatangaza msaada mpya wa karibu dola bilioni moja kusaidia vita vinavyoendelea. Naye waziri mkuuy wa Finland Mette Frederiksen alikuwa Kyiv Jumatano ambako alilihutubia bunge baada ya nchi yake pamoja na Uholanzi kuahidi kupeleka ndege 19 za mashambulizi za aina ya F-16.







