Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde amesema serikali imeanza zoezi la usambazaji wa mbolea za ruzuku

Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde amesema serikali imeanza zoezi la usambazaji wa mbolea za ruzuku mapema ili kuepukana na tatizo la ucheleshwaji wa mbolea hiyo hali inayowaathiri wakulima.

Silinde ameeleza hayo wakati alitembelea ghala la mbolea la kampuni ya YARA pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Anne Beathe Tvinnereim aliyepo nchini kushiriki Mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika na kueleza kuwa nchi yake imetoa msaada wa Dola milioni tisa za Marekani kusaidia katika usalama wa chakula nchini.   credits video @azamtvtz

 

 

 

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Dkt. Geraldine Mukeshimana pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button