LaurenLondon amepewa hisa ya Umiliki wa mali ya biashara ya marehemu
. LaurenLondon amepewa hisa ya umiliki wa mali ya biashara ya marehemu rapper NipseyHussle, London alipokea umiliki huo kutoka kwa kaka mkubwa wa rapa huyo, BlaccSam, ambaye hivi karibuni aliwasilisha ripoti ya milki ya Nipsey ambayo ina thamani ya dola milioni 11(zaidi ya Sh.Bilioni 27) kwa jumla.
.
Kulingana na ripoti hiyo, watoto wawili wa Nipsey, Emani na Kross, ndio wanufaika wake pekee na kila mmoja atapata 50% ya mali yake. Mali ya rapper huyo ina dola milioni 7 zilizosambazwa katika akaunti mbalimbali za benki, pamoja na dola milioni 4 kutoka kwa makampuni mbalimbali, Chevy Suburban ya 2012, na zaidi.







