Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amefanya mabadiliko ya uongozi katika Sekta ya Maji wilayani Rufiji.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amefanya mabadiliko ya uongozi katika Sekta ya Maji wilayani Rufiji.
Hatua hiyo inahusu uongozi katika Mamlaka ya Maji ya Utete ambapo Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Bwn. Christopher Mwigune amebadilishwa.
Mabadiliko mengine yanahusu Wakala ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) ambapo Meneja wa Wilaya hiyo kwa sasa atakuwa Mhandisi Alkam Omari ambaye pia atakaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Utete kwa mpito ambapo mamlaka hiyo itaundwa upya.

Mradi wa maji wa Chumbi mambo safi – Aweso
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amezindua mradi wa maji wa kata ya Chumbi, Rufiji mkoa wa Pwani
.
Gharama ya mradi huo ni shillingi 722,020,274.49 na unanufaisha wakazi zaidi ya elfu nane wa vijiji vitatu vya kata hiyo vya Chumbi A,B na C.







