Chadema Yageuka Mbogo Yaitisha Kamati Kuu Kujadili Uchaguzi Seriki za Mitaa

Chadema Yageuka Mbogo Yaitisha Kamati Kuu Kujadili Uchaguzi Seriki za Mitaa

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imepanga kufanya kikao cha dharura kesho, ljumaa, Novemba 29, 2024 kujadili uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji, uliofanyika nchini kote jana, Novemba 27, 2024.

Taarifa kwa umma iliyotolewa leo Alhamisi, Novemba 28, 2024 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, imesema ikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Mrema amesema kikao hicho kitajadili agenda maalumu yaliyojiri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika jana Jumatano, Novemba 27, 2024.

“Kauli ya chama itatolewa baada ya kikao hicho kumalizika,” amesema Mrema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button