Ajali ya Costa na Lori Yaua Watu 14 Mikese

Ajali ya Costa na Lori Yaua Watu 14 Mikese

Watu 14 wamefariki na wengine wanane
kujeruhiwa katika ajali iyohusisha lori la mizigo lililokuwa linatokea Dar es saalam kwenda Morogogoro na Coaster iliyokuwa inatokea Morogoro kwenda Dar es salaam
usiku huu December 18,2024 eneo la Mikese barabara kuu ya Morogoro – Dar es salaam.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mkoa Morogoro Nkungu Daniel amethibitisha kupokea kwa mili hiyo na majeruhi ambapo amesema waliofariki bado mili yao
haijatambulika.

Nkungu amesema kati ya marehemu 14 Wanaume wanane na Wanawake ni 6 huku majeruhi wakiwa wanaendelea na matibabu katika Hospitali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima, amefika Hospital ya Rufaa Mkoa Morogoro wanakopatiwa
matibabu majeruhi hao ambapo ametoa wito Wananchi kufikia katika Hospitali hiyo Ili kutambua mili ya Ndugu zao. Katika ajali hiyo Madereva wote wamefariki

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button