Squid Game Final Season Kuachiwa Leo, Juni 27

Squid Game Final Season Kuachiwa Leo, Juni 27

Wapenzi wa Filamu na Movie ulimwenguni wanajua Leo Juni 27 ndio ile siku ambayo Filamu ya SQUID GAME kutoka Korea Kusini ambayo imejizolea umaarufu ulimwenguni kote na kupendwa na watu wengi inaachiwa rasmi.

Msimu huu wa tatu wa Filamu hiyo unatarajiwa kuwa msimu wa mwisho wa Filamu hiyo ambayo iliyoachiwa rasmi kwa mara ya kwanza mwaka 2021.

Hwang Dong-Hyuk mtayarishaji wa Filamu hiyo ametoa angalizo mapema kuwa mwisho wa Filamu hiyo wa furaha kama ambavyo wengi wamezoea kuona filamu nyingi zikimalizika kwa “Happy Ending”.

“Watu hupenda mwisho wa furaha. Mimi pia ni kama wao.

Lakini baadhi ya hadithi, kwa asili, haziwezi kuwa na mwisho wa furaha. Ukijaribu kuubuni kwa nguvu, kiini cha hadithi kinaharibika. Kama hadithi inaakisi uhalisia, basi si kila mara huwa na mwisho wa furaha. Squid Game siyo tofauti.” Alisema Hwang Dong-Hyuk kwenye mahojiano yake na The Guardian.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button