“Ukisubiri Heshima Utangoja Mpaka Ukifa”Diamond

“Ukisubiri Heshima Utangoja Mpaka Ukifa” Diamond

Diamond Platnumz ameonesha hajali kile alichokiita kutopewa heshima anayostahili licha ya mafanikio yake makubwa kwenye muziki wa Afrika. Kauli yake imetokana na maoni ya shabiki aliyeonekana kumtetea na kupongeza juhudi zake kimuziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, shabiki aitwaye Rotmic24 aliandika:

“Watoto wa TZ wanakuchukia poa sana ila hawajui kua unatutebea sana kimziki bongo. Unajua mnyama SIMBAAAA

MOST SUBSCRIBED YOUTUBER IN

AFRICA NOW
Shabiki huyo alieleza jinsi Watanzania wengi wanavyoshindwa kutambua mchango mkubwa wa Diamond kwenye muziki wa Bongo, licha ya mafanikio yake makubwa kama msanii mwenye subscribers wengi zaidi YouTube (Kusini mwa Bara la Afrika).

Diamond hakusita kujibu na kuandika:

“Rotmic24 hao ni mpaka ukifa ndio wanakupa unachostahili, ukisubiri heshima muda huu utangoja sana…

Kikubwa fanya wajibu wako tu halaf kula Super Glue

Kauli hiyo inaweza kuibua mjadala mkubwa mtandaoni, ambapo mashabiki wengine wanaongeza maoni yao kuwa Diamond amekuwa akivunja rekodi nyingi lakini bado haonekani kupokea sapoti ya kutosha kutoka kwa baadhi ya Watanzania.

Kwa sasa, Diamond anaendelea kuwa mmoja wa wasanii wakubwa Afrika, akiwa na mafanikio makubwa sio tu kwenye muziki bali pia kwenye biashara na ushawishi wa kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button