Harusi ya Davido – Aliko Dangote pamoja na muigizaji nguli wa Marekani, Djimon Hounsou, ambaye kwa asili ni raia wa Benin.

Harusi ya Davido na Chioma iliyofanyika nchini Marekani imevuta hisia za watu wengi na kukutanisha mastaa wakubwa kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Miongoni mwa waliopamba tukio hilo ni tajiri namba moja barani Afrika, Aliko Dangote pamoja na muigizaji nguli wa Marekani, Djimon Hounsou, ambaye kwa asili ni raia wa Benin.

Djimon Hounsou (61) ni jina kubwa kwenye tasnia ya filamu duniani, akiwa ameigiza kwenye filamu maarufu kama Gladiator (2000), Blood Diamond (2006), na Never Back Down (2008). Mbali na mafanikio hayo, Djimon amewahi kuteuliwa mara kadhaa kuwania tuzo za filamu zenye heshima kubwa duniani Oscars.

Uwepo wake kwenye harusi hiyo ni ishara ya heshima kubwa aliyoipata Davido, na pia jinsi tukio hilo lilivyovuka mipaka ya muziki na kuwa la kidunia.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button