DKT. SAMIA AMKARIBISHA WENJE CCM

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho Ndugu Ezekia Dibogo Wenje ambaye ameamua kujiunga na CCM na kutangazwa leo Oktoba 13, 2025 katika mkutano wa Kampeni wa Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Chato mkoani Geita.

DKT. MIGIRO AMPOKEA MWANACHAMA MPYA WA CCM

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro akimpokea Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa Ndugu Ezekia Dibogo Wenje ambaye atangaza kukihama Chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa hadhara wa Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Chato Mkoani Geita leo Jumatatu Oktoba 13, 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button