Ronaldo Awapa Wachezaji Wenzake Saa za Kifahari Kama Za vadi ya Ushindi UEFA NL 2025
Ronaldo Awapa Wachezaji Wenzake Saa za Kifahari Kama Za vadi ya Ushindi UEFA NL 2025
Mastaa wa timu ya taifa ya Ureno wamepokea zawadi ya kipekee kutoka kwa nahodha wao, Cristiano Ronaldo, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea ubingwa wao wa UEFA Nations League 2025.
Ronaldo amenunua saa 35 za kifahari aina ya “Epic X 2025 UEFA Nations League Champions Edition”, moja kwa kila mchezaji, kama ishara ya kuthamini jitihada zao katika safari ya kutwaa taji hilo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa timu, kila saa imetengenezwa maalum (custom-made) kwa heshima ya kila mchezaji ikiwa na alama ya taifa la Ureno, nembo ya Seleção Portuguesa de Futebol, na mandhari ya rangi ya bendera ya Ureno. Saa hizo pia zina case ya 44mm ya chuma, skeleton hand-wound movement, pamoja na trophy ya UEFA Nations League iliyochongwa kwenye bridge.
Ronaldo, ambaye ameongoza Ureno katika mafanikio mengi kwa zaidi ya muongo mmoja, ametoa zawadi hiyo kama njia ya kushukuru mchango wa kila mmoja kwenye kikosi kilichofanikiwa kuandika historia mpya ya soka la Ulaya.
Kwa ujumla, saa 35 kwa wachezaji 35 zimetengenezwa kila moja ikiwa ni kipande adimu kinachoelezea hadithi ya ushindi wa kihistoria wa Ureno mwaka 2025.
Mashabiki duniani kote wameonyesha kuvutiwa na kitendo hicho cha ukarimu kutoka kwa CR7, wakiitafsiri kama ishara ya uongozi, umoja na moyo wa timu ambao umeifanya Ureno kuendelea kuwa moja ya timu kubwa barani Ulaya.






