Mwanaume Akamatwa Kujifanya Yeye ni Mama Yake

Mwanaume Akamatwa Kujifanya Yeye ni Mama Yake

Kisa cha kushangaza kimetikisa Italia baada ya mwanaume mwenye umri wa miaka 57 kukamatwa kwa kujifanya mama yake aliyefariki mwaka 2022 ili kuendelea kudai pensheni na kitudisha kitambulisho cha taifa cha marehemu huyo.

Tukio hilo lilifichuliwa katika mji wa Borgo Virgilio, Mantua, baada ya wafanyakazi wa ofisi ya serikali kushuku mwonekano wa “mwanamke mzee” aliyefika kuomba upya kitambulisho. Waligundua kuwa alikuwa na nywele nyeusi kwenye shingo, mikono na kidevu, na mwendo wake haukuendana na umri wa picha ya kitambulisho chazamani.

Baada ya uchunguzi wa CCTV, ilibainika kuwa “mwanamke” huyo alikuwa ni mtoto wa marehemu, ambaye anadaiwa kutumia wig, vipodozi, hereni, nguo za kike na mwendo wa kujifanya mzee ili kuficha utambulisho wake. Lengo kuu lilikuwa kuendelea kupokea pensheni ya mama yake, ambayo inakadiriwa kufikia zaidi ya €60,000 kwa kipindi cha miaka mitatu.

Polisi walipomkamata, waligundua pia mwili wa mama yake umehifadhiwa ndani ya nyumba, ukiwa umeanza kuoza bila kuzikwa ipasavyo. Hali hiyo imemfanya mshukiwa akabiliwe na mashtaka mazito kama udanganyifu, kuiga utambulisho, kuweka mwili wa marehemu nyumbani bila taarifa na jaribio la kughushi nyaraka.

Kisa hiki kimepewa jina la “Mrs. Doubtfire scandal” na vyombo vya habari, kutokana na aina ya uigizaji aliofanya mwanaume huyo. Licha ya uhalifu huo kufichuka, uchunguzi bado unaendelea ili kubaini dhamira kamili, muda halisi wa kifo na iwapo kuna mtu mwingine aliyehusika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button