Afukua Maiti na Kupeleka Bank Alipoambiwa Hawezi Kutoa Pesa Mpaka Marehemu Aende Mwenyewe

Afukua Maiti na Kupeleka Bank Alipoambiwa Hawezi Kutoa Pesa Mpaka Marehemu Aende Mwenyewe

Tukio la kushangaza limetokea nchini India ambapo mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 50 aliamua kufukua kaburi la dada yake miezi mitatu baada ya kifo chake na kubeba mabaki yake hadi benki kwa lengo la kutoa pesa zake.

Kwa Mujibu wa Indian Today Inaelezwa kuwa mwanaume huyo alifika katika tawi la benki akitaka kutoa akiba ya marehemu iliyokadiriwa kufikia takribani Tsh 650,000 hadi Tsh 700,000. Hata hivyo, maafisa wa benki walikataa maombi yake wakimtaka mmiliki wa akaunti kufika mwenyewe, pamoja na nyaraka rasmi kama cheti cha kifo na uthibitisho wa urithi.

Kutokana na kukosa uelewa wa taratibu hizo na hali ngumu ya maisha, mwanaume huyo alichukua hatua hiyo ya kushangaza ya kufukua mwili wa dada yake na kuubeba umbali wa kilomita kadhaa hadi benki akiamini angeweza kusaidiwa.

Tukio hilo liliposambaa mitandaoni lilizua mjadala mkubwa, huku likionyesha changamoto za elimu ya kifedha na ugumu wa mifumo ya benki kwa watu wa hali ya chini vijijini. Baada ya tukio hilo kuwa gumzo, benki iliripotiwa kuachia fedha hizo kwa mwanaume huyo kama mrithi pekee huku mamlaka zikichukua hatua za kumshauri na kumsaidia kisaikolojia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button