Bahati Nzuri na Bahati Mbaya kwa Yanga na Simba
Kama Simba na Yanga wanataka kwenda nusu fainali basi waombee bahati ya kutopangwa na Mamelodi Sundowns ambao wameongoza katika kundi A. Kila mmoja anaweza kupewa Mamelodi.
Yanga wana bahati kwamba wanaweza kupewa ASEC Mimosas. Lakini wanaweza kupewa Petro Atletico ya Angola. Bahati nzuri kwao ni kwamba hawawezi kupewa Al Ahly ambao walikuwa nao kundi moja. .
Bahati mbaya kwa Simba ni kwamba anaweza kupewa Al Ahly au Mamelodi. Bahati nzuri kwao ni kama ikipewa Petro Atletico.
Hawa kina Al Ahly na Mamelodi sio watu wazuri sana katika hatua za robo fainali. Kwao inakuwa kama vile michuano ndio imeanza.
Kwa Mnyama kama itatokea nafasi ya kupewa Al Ahly au Mamelodi basi ni bora wapewe Al Ahly.
Hawaonekani kuwa sawa kama walivyokuwa katika miaka ya nyuma. . Simba anaweza kupambana na Al Ahly kama alivyofanya katika michuano ya Super League.
Mamelodi ni ndoto ya kutisha. Sio Yanga wala Simba ambao wanaweza kupambana nao kwa sasa.
Petro hawana historia ya kutisha katika michuano hii na kwa upande wa ASEC itashangaza kama wanaweza kuwa timu ya kwanza ya Afrika Magharibi kufika nusu fainali tangu Enyimba walipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 2003 ambapo walikwenda moja kwa moja kuchukua taji hilo na kuwa timu ya mwisho ya Afrika Magharibi kufanya hivyo.”






