Bakari Machumu Ajiuzulu Nafasi ya Makamu Mwenyekiti TEF

Bakari Machumu Ajiuzulu Nafasi ya Makamu Mwenyekiti TEF

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu amejiuzulu nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Machumu amekabidhi barua ya kujiuzulu kwake kwa Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, leo Novemba 26, 2025, alipokutana na wahariri kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Aliteuliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, nafasi inayomhitaji kuzingatia majukumu yake mapya kikamilifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button