Dani Alves amehukumiwa kifungo cha miaka 4 na Nusu Jela baada ya kukutwa na hatia ya ubakaji, nchini Uhispania
Nyota wa zamani wa FC Barcelona na Timu ya Taifa ya Brazil, Dani Alves amehukumiwa kifungo cha miaka 4 na Nusu Jela baada ya kukutwa na hatia ya ubakaji. Alves mwenye umri wa miaka 40, amehukumiwa leo nchini Uhispania kufuatia kesi ya ubakaji ambapo anatajwa kumbaka Mwanamke mmoja kwenye Kumbi ya starehe nchini Uhispania mwaka 2022.
Mbali na hukumu hiyo, Alves ametakiwa kumlipa mwanamke huyo fidia ya (Euros 150,000) sawa na zaidi ya TSh. Milioni 415







