Dkt.Mwigulunchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bi. Elke Wisch

Waziri wa @urtmof Dkt. @mwigulunchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bi. Elke Wisch, aliyeambatana na ujumbe kutoka Shirika hilo, jijini Dodoma, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya maendeleo na ushirikiano ikiwemo namna ambavyo Tanzania inavyofanya vizuri katika masuala ya bajeti.

Bi. Elke Wisch ametumia fursa hiyo pia kumkabidhi Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), baadhi ya machapisho ya Shirika hilo yanayohusu Utafiti wa Utekelezaji wa Bajeti (Budget Survey).

Kikao hicho kimedhuriwa pia Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha, , Bi. Amina Khamis Shaaban na Bw. Elijah Mwandumbya, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje. Bw. Rished Bade, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Bajeti, Bi. Vicky Jengo na maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button