Habari kubwa leo ni kuhusu R.Kelly kuzidishiwa dawa hospitali ya Magereza hali iliyopelekea awahishwe Hospitali ya Umma kwa ajili ya kunusuru uhai wake,
Habari kubwa leo ni kuhusu R.Kelly kuzidishiwa dawa hospitali ya Magereza hali iliyopelekea awahishwe Hospitali ya Umma kwa ajili ya kunusuru uhai wake, kufuatia sakata hilo Wakili wa msanii maarufu wa R&B, R. Kelly, Beau Brindley, amedai kuwa mteja wake amelazwa hospitali baada ya kupewa dozi kubwa ya dawa ambayo ilihatarisha maisha yake, katika kile anachokieleza kuwa ni jaribio la kumuua akiwa gerezani.
Brindley amesema: “Wapo waliodhani kuwa haiwezekani kwa Maafisa wa Idara ya Magereza kupanga kumuua R. Kelly, lakini matendo ya wazi ya maafisa hao hivi sasa yanaonyesha mpango huo upo na unaendelea kutekelezwa.” Wakili huyo anadai kuwa hospitali ya gereza ilimpa R. Kelly kiasi kikubwa cha dawa ambacho kingeweza kumuua, huku pia wakisimamisha matumizi ya dawa za kupunguza damu kuganda , licha ya msanii huyo kuwa na matatizo ya kuganda kwa damu kwenye mapafu.
Brindley ameendelea kudai kuwa maafisa wa magereza walimtoa R. Kelly kwenye chumba cha upasuaji ambao ungeweza kuokoa maisha yake wakiwa na silaha na kumpeleka kwenye selo ya binafsi , jambo ambalo linahatarisha maisha yake.
“Walimtoa hospitalini kwa kutumia bunduki na kumrudisha kifungoni akiwa bado na damu iliyoganda kwenye mapafu. Walitaka R. Kelly afe kabla ya ukweli kuhusu uhalifu aliofanyiwa katika kesi zake kufichuliwa,” alisema Brindley.
Wakili huyo sasa ametoa wito kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, kuingilia kati. “Tunamuomba rais asiwaruhusu watu hawa kutekeleza mpango huu. Aokoe maisha ya mtu.”
Kwa upande wao, Idara ya Magereza nchini Marekani imeeleza: “Kwa sababu za faragha, usalama na ulinzi, hatuwezi kutoa taarifa kuhusu hali ya kifungo cha mfungwa yeyote, ikiwemo masuala ya kiafya.”
R. Kelly amekuwa gerezani tangu mwaka 2022, akitumikia kifungo cha miaka 30 kwa makosa ya uhalifu wa kupanga (racketeering) na usafirishaji wa kingono wa watu (Sex )






