Hakuna Msanii Asiye Adhirika na Hasira za Wananchi.
Hakuna Msanii Asiye Adhirika na Hasira za Wananchi
Dogo Paten amefunguka kuhusu hali ngumu inayokikumba kiwanda cha muziki nchini, akieleza kuwa hakuna msanii ambaye hajaathirika na hasira za mashabiki kufuatia yaliyojiri hivi karibuni. Akizungumza na @saditz_official, Dogo Paten amesema hali hiyo imeathiri wasanii wote bila ubaguzi, hasa upande wa shoo za majukwaani.
Akijibu swali la nini kimempa ujasiri wa kuachia wimbo mpya kipindi ambacho baadhi ya wasanii wanaogopa, Dogo Paten amesema ameona ni wakati sahihi kuachia “Nishike Mkono” kwa kuwa ujumbe wake unaendana moja kwa moja na hali ya sasa. Kwa mujibu wake, wimbo huo ni maombi na kilio cha ndani kinachoakisi hisia za wengi katika kipindi hiki kigumu.
“Hakuna msanii ambaye hajaathirika na yaliyotokea, show hakuna,” amesema Dogo Paten, akisisitiza kuwa hali ya mashabiki imegusa uchumi na morali ya wasanii wengi.
Kauli hiyo inaonesha wazi changamoto iliyopo baina ya wasanii na mashabiki, huku baadhi ya wasanii wakitafuta njia za kuendelea kuwasiliana na jamii kupitia sanaa yenye ujumbe unaogusa hali halisi ya wakati uliopo.





