Huu ni Uchaguzi Wakuamua Neema au Maumivu kwa Watanzania.

Huu ni Uchaguzi Wakuamua Neema au Maumivu Kwa Watanzania.

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu, amesema akifanikiwa kuingia madarakani katika uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, ataongoza Serikali yenye uadilifu na bila hofu ya vyombo vya habari.

“Serikali tunayokwenda kuunda kupitia Chaumma, ambayo nitakwenda kuiongoza, sina hofu wala shaka ya kuogopa kukosolewa iwe ndani au nje, iwe mvua au jua, iwe mchana au usiku. Kwa sababu nakwenda kuunda na kuongoza Serikali safi iliyojaa uadilifu, hivyo tasnia ya habari mjiandae,” amesema Mwalimu.

Mwalimu ametoa kauli hiyo leo Jumapili, Agosti 31, 2025, wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chaumma uliofanyika katika Viwanja vya Biafra, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button