Iran Imemnyonga Leo Asubuhi Jasusi Mwingine wa Israel

Iran Imemnyonga Leo Asubuhi Jasusi Mwingine Wa Israel

Mamlaka ya Iran imemuua kwa kumnyonga raia wake ambaye ni kijana mmoja aitwaye Mohammadamin Mahdavi-Shayesteh kwa kufanya makosa ya kuofanyia ujasusi Israel huko nchini Iran Jasusi huyo wa Israel amenyongwa leo siku ya Jumatatu asubuhi, chombo cha habari cha mahakama cha Iran kiliripoti.

“Kwa mujibu wa nyaraka za kesi, alikuwa kiongozi wa mtandao wa mtandao unaohusishwa na Mossad na alikuwa akijua kushirikiana na ujasusi wa utawala wa Kizayuni,” idara ya mahakama ilisema.

Jasusi huyo alikuwa akifanya kazi kwenye Shirika lisilo la kiserikali lililopo chini Iran ambalo ni la Haki za Kibinadamu mashtaka dhidi yake ni pamoja na “kutusi mambo matakatifu ya Kiislamu” na “kushirikiana na adui.”

Taarifa hiyo Iliongeza kuwa hukumu ya kifo ilitolewa kufuatia kukiri kufanya makosa yote aliyotuhumiwa nayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button