Je Wajuwa Siri ya Myama Pundamilia ?

MISTARI KWENYE MWILI WA MNYAMA PUNDAMILIA.
Ushawahi kujiuliza pundamilia ana rangi gani? Ni mweupe mwenye mistari myeusi au ni mweusi mwenye mistari myeupe?

Hili swali limesumbua wengi sana, ila wataalamu wa wanyama baada ya kupata shida muda mrefu na kuchunguza kwa kina, wakaja na jibu wakisema “Pundamilia ni mnyama mweusi mwenye mistari myeupe”. Hapo vipi? 😃🙌

NGOJA NIELEZEE KWA UCHACHE HILI NA KWA LUGHA RAHISI.
Kwa wanyama wote, kuna seli ambazo hujulikana kama MELANOCYTES CELLS ambazo ndo huhusika na uzalishaji wa ile MELANIN (Melanin-pigment) inayohusika na rangi kwenye ngozi.

Hii melanin inapokosekana kwenye ngozi ya pundamilia, ndo ile sehemu ya mstari mweupe unatokea. Kama utamchuna pundamilia manyoya yote mwilini, utakutana na ngozi yenye rangi nyeusi.

Kwa lugha rahisi ni kuwa “Ule msitari mweupe ni umetokana na kukosekana kwa melanin kwenye ile sehemu (Pigment is denied)”. Hii hata kwa binadamu huwa ipo, ndo ikikosekana inasababisha tunapata watu wenye ulemavu wa ngozi kama albino (Albinism) japo hata kwa wanyama hii albinism pia ipo.

MISTARI YA PUNDAMILIA HUMSAIDIA NINI AU NI KAMA UREMBO?
Mistari ya pundamilia ina mambo mengi kwake na machache kati ya mengi ni kama ifuatavyo;-

1. KUWACHANGANYA ADUI ZAKE.
Hii humsaidia kuwachanganya wanyama wala nyama hasa wakiwa wanamuwinda kwakuwa hushindwa kumlenga mmoja wa kumkamata. Pia akiwa kwenye nyasi anakuwa haonekani vizuri (camouflage).

2. KUMKINGA NA WADUDU WASUMBUFU.
Mistari pia inamsaidia kujikinga na wadudu kama mbung’o na wengine wanaong’ata maana hupata sana shida kutua kwenye mwili wake kutokana na muonekano wa ile mistari. Hivyo humkinga na magonjwa.

3. UTAMBULISHO.
Mistari ya pundamilia ni ya kipekee, ni kama alama za vidole (fingerprints) na haifanani kamwe baina ya wanyama wawili. Hii husaidia kutambuana wao kwa wao hasa wale wa jamii moja, au mama na mtoto wake, n.k.

4. KUSHARABU NA KUAKISI MWANGA.
Hapa sasa nakurudisha shule ya msingi 😃. Mwalimu wako wa sayansi alikwambia rangi nyeusi na nyeupe kwenye mwanga inafanya kazi gani? Kwanini shuleni mliambiwa mvae mashati meupe na sio meusi? Kama umesahau, mrudishie mzazi wako ada yake acha wizi na janja janja. 🤕

 

 

Group of zebras in Tarangire National Park / Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button