Jenista Muhagama Afariki Dunia

Jenista Muhagama Afariki Dunia

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho Jenista Joakim Mhagama, kilichotokea leo December 11, 2025 Jijini Dodoma.

“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kilichotokea leo 11 Jesemba, 2025 Jijini Dodoma, natoa pole kwa Waheshimiwa Wabunge wote amilia ya Marehemu, ndugu, jamaa na Wananchi wa Jimbo la Peramiho Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu”

“Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa, Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi, Amina”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button