Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linafanya uchunguzi wa tukio la mauaji ya Costa Clemence (22) Mjasiriamali na Mkazi wa Maseyu
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linafanya uchunguzi wa tukio la mauaji ya Costa Clemence (22) Mjasiriamali na Mkazi wa Maseyu ambaye alikutwa ameuawa katika Kijiji hicho kilichopo Kata ya Gwata Tarafa ya Mikese Wilaya ya Morogoro.
Kwa mjibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani humo, tukio hilo limetokea Septemba 15, 2024 huko eneo la Maseyu katika eneo ambalo halina Makazi ya watu na pembeni yake kukiwa na pikipiki ambayo haina namba za usajili inayosadikiwa kuwa ni mali ya marehemu.
Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wanaoishi jirani na eneo hilo na yeyote mwenye taarifa kuhusiana na tukio hilo asisite kuwasiliana na Polisi au Mamlaka yoyote anayoona inafaa ili kufanikisha kuwakamata wahusika wa tukio hilo.






