Karatu: padri auawa na mtu aliyeenda kuomba aombewe

Tukio limetokea usiku wa kuamkia Julai 19, 2023 Mkoani #Arusha, ikielezwa mtuhumiwa ambaye jina lake halijatambulika alienda
Kanisani kumgongea mlango Padri Pamphilius Nada wa Parokia ya Karatu ili amuombee.
Baada ya Padri kufungua mlango mtu huyo akamvamia na kumpiga kwa Nyundo kichwani, kitendo ambacho kilikatisha uhai wa Kiongoz huyo muda mfupi baadaye Kamanda wa Polisi, Justine Masejo, amesema.
“Mtuhumiwa inadaiwa alikuwa na changamoto ya Afya ya Akili, naye alifariki
baada ya kushambuliwa na Wananchi eneo la tukio.”
#Bongplus updates





